SURA YA TATU
III. HESABU NA ALAMA YA MNYAMA
Mambo mawili makuu sana ya mamlaka hii ya Mnyama yanafunuliwa katika Ufunuo 13. "Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe CHAPA [ALAMA] katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa [alama] ile, yaani, jina la Mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya Mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita." Ufunuo 13:16-18. Mpaka hapa katika somo letu tumezieleza ishara zile tisa za kuitambulisha mamlaka hii ya Mnyama na kuzitumia kwa Upapa. Hapa tutaongeza pointi ya KUMI katika orodha yetu kwa ajili ya kuifafanua hesabu hii ya jina lake.
Kwa mujibu wa Ufunuo 13:17, hesabu ya jina lake itakuwa pia ni hesabu ya mwanadamu. Bila shaka inamhusu mtu yule anayeiongoza mamlaka ile ya Mnyama. Njia ya zamani ya kuipata hesabu ya jina ni kuchukua thamani ya tarakimu za herufi zote na kuzijumlisha ili kupata jumla yake. Kama tunataka kutumia kipimo hicho kwa Upapa, yatupasa kupata jina la kiofisi [cheo] la Papa, ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo. Kama hiyo ni hesabu ya mtu, basi, bila shaka ingekuwa ni ya mtu yule anayeuongoza mfumo ule [wa dini].
Ni jambo la kuvutia macho kuona kwamba kuna cheo rasmi cha Kilatini cha Papa, cheo ambacho amepewa na Kanisa lenyewe. Cheo hicho kinaonekana tena na tena katika vitabu vya Kanisa la Roma. Lakini katika gazeti la kila juma la Kikatoliki liitwalo, OUR SUNDAY VISITOR, la Aprili, 1915, tunao usemi wa kuvutia unaosema kwamba herufi ya cheo hicho rasmi zimeandikwa katika kofia yake ya Kiaskofu (miter or mitre). Hapa ni dondoo lenyewe: "Herufi zilizoandikwa katika kofia ya Papa ni hizi; VICARIUS FILII DEI, ambacho ni Kilatini cha 'ALIYE BADALA YA MWANA WA MUNGU' (VICAR OF THE SON OF GOD). Wakatoliki wanashikilia [wanaamini] kwamba Kanisa ambalo ni jamii inayoonekana ni lazima liwe na kichwa kinachoonekana; Kristo kabla ya kupaa kwake kwenda mbinguni, alimchagua Mtakatifu Petro kuwa kama Mwakilishi wake. Kwa hiyo, Askofu wa Rumi kama kichwa cha Kanisa, alipewa cheo cha 'Aliye Badala ya Kristo' (Vicar of Christ)." Kwa siku hizi kofia ya papa [tiara] haina cheo chake cha Kilatini, lakini maneno hayo yanatumika katika sherehe za kumtawaza kila Papa mpya anayevikwa taji [kofia hiyo].
Basi, tukiwa na cheo hiki rasmi cha Papa mkononi mwetu, tunaweza kuendelea kutumia kipimo hiki cha Maandiko haya. Tunaipataje hesabu ya jina lake? Kwa kupata thamani ya tarakimu za Kirumi za cheo chake cha VICARIUS FILII DEI, tunaifikia hasa hesabu hiyo halisi, 666. Angalia jinsi hesabu hizo zilivyofanywa hapa chini, kila herufi ikipewa thamani ya tarakimu yake:
V ----- 5 F ----- 0 D ----- 500 112
I ----- 1 I ----- 1 E ----- 0 53
C ----- 100 L ----- 50 I ----- 1 501
A ----- 0 I ----- 1 ___ ___
R ----- 0 I ----- 1 501 666
I ----- 1 ___
U au V ----- 5 53
S ----- 0
____
112
Mmoja anaweza kubisha kwamba hilo linaweza kuwa ni jambo linaloweza kutokea kwa nasibu. Tunakubali ya kwamba upo uwezekano kwa jambo kama hilo kutokea kwa nasibu tu, kama tungekuwa na pointi moja hiyo tu ya utambulisho ya kuitegemea. Lakini, basi, ukweli ni kwamba, hiyo ni pointi ya KUMI miongoni mwa orodha ndefu ya ishara za tabia yake ambazo Biblia huzitumia kuitambulisha mamlaka hiyo ya Mnyama. Hii inaongezea tu uzito na nguvu kwa yale ambayo tayari yamekwisha kusemwa kwa kuzitumia [ishara zile] kuionyesha mamlaka hiyo ya Papa. Ni uthibitisho wa kilele pamoja na zile ishara nyingine zote zilizowekwa kwa wazi sana katika Maandiko.
ALAMA HII ----- NI UDANGANYIFU MKUU
Sasa tuko tayari kuchukua hitimisho la kilele cha udanganyifu huu kwa kadiri mamlaka hiyo ya Mnyama huyo inavyohusika. Tayari tumekwisha jifunza ya kwamba mamlaka hii ingeweka mafundisho mengi ya uongo kinyume na mafundisho makuu ya kweli zake Mungu. Kwamba [mamlaka hiyo] ilikuwa ni mchanganyiko wa mawazo ya kipagani na mafundisho ya dini ya Kikristo ambayo yamekusanywa pamoja kwa hali inayoleta machafuko [kuchanganyikiwa], yanayoitwa vyema kama "BABELI" katika Maandiko.
Mafundisho machache ya uongo yanaweza kuorodheshwa kama ifuatavyo: badala ya Neno la Mungu, imeweka MAPOKEO; badala ya Roho Mtakatifu, imemweka PAPA; badala ya toleo moja tu la Kristo, imeweka MISA [toleo la kila siku]; badala ya ubatizo, imeweka KUNYUNYIZA; badala ya Meza ya Bwana, imeweka MKATE UNAOBADILIKA KABISA NA KUWA MWILI NA DAMU HALISI YA YESU (Transubstantiation); badala ya Sheria ya milele ya Mungu, imeweka SHERIA ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO [Amri Kumi]; badala ya Zaka; imeweka KODI [Ushuru] na INDULGENSIA [kuuza vyeti vya msamaha wa dhambi]; badala ya mauti, imeweka MAHALI PA KUTAKASIA DHAMBI au TOHARANI (Purgatory); badala ya Muhuri wa Mungu, imeweka ALAMA [CHAPA] YA MNYAMA.
Hapa tunashughulika hasa na ALAMA YA MNYAMA. Katika Ufunuo 14:9,10 tunasoma hivi, "Mtu awaye yote akimsujudu huyo Mnyama na Sanamu yake, na kuipokea chapa [alama] katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake." Hili ni jambo la KUFA NA KUPONA. Ni lazima tujue kabisa alama hii ni ya kitu gani hasa na jinsi tunavyoweza kuikwepa.
Kwanza tunaona katika Biblia ya kwamba ALAMA hii daima iko kinyume na MUHURI WA MUNGU. Katika Ufunuo 7:2,3, tunajifunza ya kwamba Muhuri wa Mungu unawekwa juu ya kipaji cha uso sawasawa tu na ile Alama ya Mnyama inavyowekwa juu ya vipaji vya uso. Vitu hivyo viwili [Muhuri wa Mungu na Alama ya Mnyama] vinaonekana kuhitilafiana moja kwa moja na kila kimoja kiko kinyume na kile kingine. Vyote viwili vinapokewa katika kipaji cha uso na mkononi. Sasa tutauliza swali, "Je, Muhuri ni kitu gani?" Kama tutalithibitisha jambo hili, basi, litatusaidia kuitambua Alama [ya Mnyama].
MUHURI WA MUNGU
Muhuri ni kitu fulani kinachohusika na mambo ya kisheria. Hati za kiserikali zikuzote zinapigwa muhuri wa mamlaka inayotawala. Kila Serikali inao muhuri ambao unagongwa katika hati zake za kisheria. Kusudi lake ni kuonyesha kwamba kuna mamlaka inayohusika nyuma ya hati ile. Hii ni kweli hasa kuhusiana na sheria za nchi. Kila sheria mpya ina muhuri kuonyesha ya kwamba nyuma yake kuna uwezo na mamlaka kuiunga mkono Sheria hiyo.
Zingatia kwamba kila muhuri una mambo matatu ndani yake. Hauna budi kuwa na JINA la mwenye mamlaka, OFISI au CHEO cha mwenye mamlaka, na ENEO analotawala. Muhuri wa Rais wa Amerika una maneno yafuatayo: Richard M. Nixon, Rais [l977], Marekani (U.S.A.). Muhuri ule unapowekwa juu ya sheria au hati ya Serikali, huonyesha kwamba mamlaka ya Rais inaunga mkono tangazo lile.
Je, Muhuri wa Mungu unahusika na Sheria Yake pia? Kama ndivyo, kwa jinsi gani na wapi unawekwa? Hebu na tusome Isaya 8:16, "Ufunge huo ushuhuda, UKAITIE MUHURI SHERIA kati ya wanafunzi wangu." Hii inathibitisha kwamba muhuri huo unahusiana na sheria. Kwa kweli, Sheria inatiwa muhuri kati ya wanafunzi wa Mungu. Lakini, je! ni wapi inapowekwa hasa Sheria hiyo kwa wale walio waaminifu? Jibu linapatikana katika Waebrania 10:16, "Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika."
Basi, hivyo ndivyo muhuri wa Bwana unavyotiwa juu ya wanafunzi Wake. Unaandikwa mioyoni mwao ama, kwa mfano, juu ya vipaji vya nyuso zao. Mithali 7:2,3 inaliweka jambo hilo wazi zaidi, "Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako." Unaona ya kwamba sheria hiyo inashikwa kwa mkono na kwa moyo; hivyo, inanenwa kwamba inatiwa mkononi na juu ya kipaji cha uso.
ISHARA YA MAMLAKA YA MUNGU
Tunataka kuchunguza katika Sheria ya Mungu kuona ni sehemu ipi hasa iliyo na Muhuri huo. Lakini, kwanza, hebu na tutafute ni kitu gani kinachoonyesha Uweza wa Mamlaka ya Mungu. Rais anayatumia mamlaka yake kwa ajili ya Cheo chake kama Rais. Mungu anadai Uweza wake kutegemea Cheo chake kama MUUMBAJI wa ulimwengu. Angalia maneno haya yanayopatikana katika Yeremia 10:10,11. "Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; ... Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu. Ameiumba dunia kwa Uweza Wake." Tena, katika Zaburi 96:5, "Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu." Weka pamoja na mafungu haya fungu moja zaidi linalopatikana katika Isaya 40:25,26, "Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi?"
Tunashawishika kuona kwamba kitu kikuu kinachomtofautisha Mungu wa kweli ni Uweza wake wa Uumbaji. Anajenga madai ya mamlaka yake kama Mungu wa kweli na wa pekee juu ya UWEZA WAKE WA KUUMBA. Lakini, je, ishara au kumbukumbu ya Uumbaji Wake ni ipi? Mwanzo 2:2,3 inatoa jibu: "Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya." SABATO ni kumbukumbu ya uweza wa uumbaji wake ambao unamtofautisha [Mungu] na miungu ya uongo.
ISHARA YA MAMLAKA YA MUNGU
Tunataka kuchunguza katika Sheria ya Mungu kuona ni sehemu ipi hasa iliyo na Muhuri huo. Lakini, kwanza, hebu na tutafute ni kitu gani kinachoonyesha Uweza wa Mamlaka ya Mungu. Rais anayatumia mamlaka yake kwa ajili ya Cheo chake kama Rais. Mungu anadai Uweza wake kutegemea Cheo chake kama MUUMBAJI wa ulimwengu. Angalia maneno haya yanayopatikana katika Yeremia 10:10,11. "Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; ... Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu. Ameiumba dunia kwa Uweza Wake." Tena, katika Zaburi 96:5, "Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu." Weka pamoja na mafungu haya fungu moja zaidi linalopatikana katika Isaya 40:25,26, "Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi?"
Tunashawishika kuona kwamba kitu kikuu kinachomtofautisha Mungu wa kweli ni Uweza wake wa Uumbaji. Anajenga madai ya mamlaka yake kama Mungu wa kweli na wa pekee juu ya UWEZA WAKE WA KUUMBA. Lakini, je, ishara au kumbukumbu ya Uumbaji Wake ni ipi? Mwanzo 2:2,3 inatoa jibu: "Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya." SABATO ni kumbukumbu ya uweza wa uumbaji wake ambao unamtofautisha [Mungu] na miungu ya uongo.
MUHURI KATIKA SHERIA
Sasa tuko tayari kuichunguza Sheria ya Mungu ili kuutafuta Muhuri wa Mamlaka Yake na kujua ni kitu gani hasa. Kumbukeni ya kwamba muhuri ni lazima uwe na JINA, CHEO, na ENEO LA UTAWALA. Tunaichunguza amri moja moja katika zile Amri Kumi za Sheria ya Mungu. Kwa taratibu zinaisha zote kasoro moja. Masharti yale matatu ya muhuri yatapatikana tu katika [amri] ile iliyo na Jina, Cheo, na Eneo la Mungu [analotawala].
Katikati kabisa ya Sheria hii ipo kumbukumbu ya Uweza Wake wa Uumbaji, na tazama, katika amri ile ya NNE tunaziona sehemu tatu za muhuri. "Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako. (Jina [BWANA= YEHOVA]) ... Maana, kwa siku sita BWANA ALIFANYA (Cheo - MUUMBAJI) mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo (Eneo analotawala), akastarehe siku ya saba." Kutoka 20:8-11. Kwa maneno mengine, SABATO NI MUHURI WA MUNGU ----- ALAMA ya Mmoja pekee awezaye kuumba na ambaye amepewa mamlaka ya kuitawala nchi hii. Tena ili kuifanya Sheria hiyo iwe na nguvu, ameweka Muhuri ndani yake, kuonyesha kwamba Yeye [Mungu] anasimama nyuma ya kila amri moja moja katika Sheria hiyo [ya Amri Kumi].
Waweza kuuliza, "Je, hivi Sabato ni Muhuri wa Mungu kweli?" Hebu na tuangalie katika Ezekieli 20:12. "Tena naliwapa Sabato zangu, ziwe ISHARA kati ya Mimi na wao, wapate kujua ya kuwa Mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye." Hapa Sabato inaitwa "ISHARA" ya Mungu. Je, [ishara] hiyo ni sawasawa na muhuri? Warumi 4:11 hufunua kwamba "MUHURI" na "ISHARA" ni kitu kile kile kimoja, maneno hayo hutumika kwa kubadilishana. "Naye aliipokea DALILI [ISHARA] hii ya kutahiriwa, MUHURI wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa."
MUHURI NA ALAMA VINASHINDANA
Hebu na tuone ni uhusiano gani upo kati ya MUHURI WA MUNGU na ALAMA YA MNYAMA. Vitu hivyo viwili vinashindana. Katika Ufunuo 14:9,10, Ujumbe wa Malaika wa Tatu unawafunua wale walio na alama [chapa] hiyo: "Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo Mnyama na Sanamu yake, na kuipokea chapa [alama] katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo."
Katika fungu la kumi na mbili tunalo kundi jingine linalotambulishwa kwa maneno haya, "Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu." Kwa maneno mengine, wale WANAOZISHIKA AMRI [KUMI] ZA MUNGU hawana Alama ya Mnyama na wale walio na Alama ya Mnyama HAWAZITII AMRI [KUMI] ZA MUNGU [Yakobo 2:10-12; Kutoka 20:3-17]. Amri hizo Kumi, zilizo na Muhuri wa Mungu, zinawekwa katika mashindano na Alama ya Mnyama. MUHURI ni SABATO, kwa hiyo SABATO ni kinyume na ALAMA hiyo [ya Mnyama]. Basi, je! alama hiyo ni nini?
JARIBIO LA KUFANYA MABADILIKO
Kulijibu swali hilo [juu] tunaelekezwa nyuma tena kwa Danieli 7:25, ambako Upapa unaelezwa kuwa ni mamlaka ile itakayo"azimu kubadili majira na Sheria." Tumekwisha jifunza tayari jinsi amri ya pili ilivyoondolewa na jinsi amri ya kumi ilivyogawanywa katika sehemu mbili katika Katekisimu za Upapa. Lakini, je! ni vipi kuhusu "majira" yaliyotajwa katika Sheria hiyo? Ni katika Amri ile ya Nne. Je, Upapa uliazimu [ulifikiria] kubadili Sabato, ambayo ni majira pekee yaliyowekwa katika Sheria hiyo? Ndio, ulifanya hivyo, na jambo hilo lilitokea kwa njia ya kushangaza.
Wapagani walikuwa na mfumo wao wa dini uliojengwa juu ya ibada ya sanamu. Siku yao takatifu ilikuwa ni siku ile ya kwanza ya juma, ambayo iliitwa Siku ya Jua (Sun-day) kwa heshima ya Mungu-jua. JUMAPILI [SUNDAY] iliadhimishwa na wapagani kinyume na uadhimishaji wa SABATO kwa Wakristo. Lakini katika siku za Mfalme wa Rumi, Konstantino, jambo kubwa lilitokea. Konstantino alidai kwamba yeye alikuwa ameongoka na kuwa Mkristo, naye akaifungua wazi milango ya Kanisa kwa wafuasi wake wote wa kipagani.
Ili kujipatia uwezo, akazikubali desturi nyingi za ibada ya jua kutoka kwa wapagani wale. Maafikiano haya mengi ya kulegeza masharti, kama vile Krismasi na Ista(Easter) [Pasaka] yamekwisha kuelezwa. Nyingine katika desturi hizo ni uadhimishaji wa Jumapili. Ilionekana inafaa zaidi kuwaruhusu wapagani kuitunza siku yao wenyewe ya ibada katika siku ile ya Jumapili, na kuwaomba Wakristo kuungana nao katika kuitunza. Kwa hiyo, Konstantino ndiye hasa aliyeitoa amri ya kwanza ya kuitunza Jumapili badala ya Sabato. Mabaraza ya Kanisa la Kipapa yakaiimarisha sheria ile mpaka ikawa imeotesha mizizi kabisa katika Ukristo na Ulimwengu.
USHUHUDA WA HISTORIA
Tukigeukia sasa kwenye ushuhuda wa wanahistoria wa kidunia, unaweza kusoma ukweli wa mambo hayo wewe mwenyewe. Kila usemi umefafanuliwa wazi katika kumbukumbu za historia. Kutoka katika Encyclopedia Brittanica chini ya kichwa 'SUNDAY' tunasoma hivi: "Alikuwa ni Konstantino aliyetoa kwanza sheria ya utunzaji sahihi wa Jumapili, na ambaye ... aliagiza kwamba ingekuwa inasherehekewa daima katika Dola yote ya Kirumi." Hapa yapo maneno ya Dkt. Gilbert Murray, M.A., D.Litt., L.L.D., F.B.A., profesa wa Lugha ya Kigiriki katika Chuo Kikuu cha Oxford: "Sasa kwa vile Mithra (Mithras) alikuwa ni 'Jua, Asiyeshindikana,' na Jua lilikuwa ni 'Nyota ya Kifalme,' dini hiyo ikamtafuta mfalme ambaye ingemtumia kama mwakilishi wa Mithra hapa duniani... Mfalme wa Kirumi alionekana wazi kwamba ndiye aliyesondwa kidole kuwa mfalme wa kweli. Kinyume kabisa na Ukristo, Umithra (Mithraism) ulimtambua Kaisari kuwa ndiye mchukuzi wa Neema, na wafuasi wake walijaa katika majeshi na idara za Serikali... Ilikubalika sana [dini hiyo] hata ikaweza kuulazimisha ulimwengu wa Kikristo kuipokea siku yake ya jua (Sun-Day) badala ya Sabato, sikukuu yake ya kuzaliwa jua, tarehe ishirini na tano ya Desemba, kama ndiyo siku ya kuzaliwa Yesu." HISTORY OF CHRISTIANITY IN THE LIGHT OF MODERN KNOWLEDGE.
Dkt. William Frederick anasema ukweli ule ule wa historia: "Mataifa yalikuwa ni watu wenye kuabudu sanamu ambao waliliabudu jua, na Jumapili (Sunday) ilikuwa ndiyo siku yao takatifu sana. Sasa, ili kuwafikia watu katika nyanja hii [ya dini], linaonekana kuwa ni jambo la kawaida tu, na la lazima, kuifanya Jumapili kuwa siku ya mapumziko ya Kanisa. Wakati huu lilikuwa ni jambo la maana kwa Kanisa ama kuichagua siku ya Mataifa, ama kuwafanya Mataifa hao kubadili siku yao. Kuibadili siku ya Mataifa lingekuwa ni chukizo na kipingamizi kwao. Kwa kawaida Kanisa lingeweza kuwafikia vizuri zaidi [Mataifa wale] kwa kuitunza siku yao." SUNDAY AND CHRISTIAN SABBATH, uk. 169, 170.
Gazeti la North British Review linatoa sababu zifuatazo kwa kuichagua siku ya wapagani ya Jumapili (Sun-day): "Siku ile ile hasa ilikuwa ni siku ya jua (Sunday) ya majirani zao wapagani na wananchi kwa jumla, na uzalendo wao ukawaunganisha kwa furaha na kwa kuzingatia manufaa ya kuifanya [siku hiyo] pasipo kuchelewa kuwa siku yao ya Bwana na Sabato yao... Kanisa lile la zamani, kwa kweli, lilifungwa kwa kuichagua Jumapili ----- mpaka hapo ilipojizatiti na kuwa [siku] kuu kabisa, wakati ilipokuwa imechelewa mno kufanyiwa badiliko jingine." Gombo la XVIII, ukurasa 409.
UKATOLIKI UNAKIRI
Kwa kuwa unabii wa Danieli ulitabiri kwamba Upapa unge"azimu" kubadili "majira na sheria" hebu na tuulize kama ulihusika na badiliko hilo la Sabato. Tunataka kufanya haki kwa kila mmoja, na kupata ushuhuda wa kweli kutoka kwa wote. Madondoo kadhaa yafuatayo yamechukuliwa kutoka kwa mamlaka zinazoaminika za Kikatoliki ambazo zinaeleza kwa wazi madai ya Upapa kuhusu jaribio hilo lililofanyika. Kutoka katika CATHOLIC ENCYCLOPEDIA, Gombo la IV, ukurasa 153, "Kanisa... baada ya kuibadili siku ya mapumziko kutoka Sabato ya Wayahudi, au siku ya saba ya juma, kwenda siku ya kwanza, likaifanya amri ya tatu kumaanisha Jumapili kuwa ndiyo siku itakayotakaswa kama Siku ya Bwana."
Gazeti la CATHOLIC PRESS, (Sydney, Australia) la Agosti 25, 1900 linalielezea jambo hilo kwa maneno haya: "Jumapili imewekwa na Wakatoliki, na madai yake ya kuitunza yanaweza kutetewa tu kwa kanuni za Kikatoliki... Tangu mwanzo wa Maandiko mpaka mwisho hakuna kifungu hata kimoja kinachoidhinisha uhamisho wa siku ya juma ya ibada kutoka siku ya mwisho ya juma kwenda ile ya kwanza." Gazeti la CATHOLIC MIRROR la Septemba 23, 1894 linaliweka suala hilo kwa njia hii: "Kanisa Katoliki kwa zaidi ya miaka elfu moja kabla ya kuwako Mprotestanti, kwa nguvu ya utume wake, lilibadili siku toka Jumamosi kwenda Jumapili."
Hapa kuna semi kutoka katika Katekisimu mbili kuonyesha madai ambayo tunayajadili: Kutoka katika THE CONVERT'S CATECHISM OF CATHOLIC DOCTRINE, by Rev. Peter Geiermann,
"SWALI ----- Sabato ni siku gani?
"JIBU ----- Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
"SWALI ----- Kwa nini tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi?
"JIBU ---- Tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki, katika Baraza la Laodikia (336 B.K.) lilihamisha taratibu ya ibada kutoka Jumamosi kwenda Jumapili." ----Toleo la Pili, uk. 50.
Rev. Stephen Keenan katika DOCTRINAL CATECHISM yake anayo haya ya kusema:
"SWALI ----- Unayo njia nyingine yo yote ya kuthibitisha kwamba kanisa linao uwezo wa kuanzisha sikukuu ambazo zinashikwa kama amri?
"JIBU ----- Kama lisingekuwa na nguvu kama hizo, lisingaliweza kufanya kile ambacho wanadini wote wa siku hizi wanakubaliana nacho ----- lisingaliweza kuweka utunzaji wa Jumapili siku ya kwanza ya juma mahali pa utunzaji wa Jumamosi siku ya saba, badiliko ambalo halina Maandiko yo yote yanayolipa kibali hicho." ----- Ukurasa 174.
Tafadhali zingatia neno "kuweka mahali pa," usemi ambao tumeutumia tena na tena kuelezea shughuli za mamlaka hii.
Katika kitabu chake cha QUESTION BOX, uk.179, Kadinali Gibbons anatoa ungamo hili la kushangaza: "Iwapo Biblia ndiyo kiongozi peke yake kwa Mkristo, basi, Mwadventista wa Sabato ana HAKI kuitunza JUMAMOSI pamoja na Myahudi ... Je, si jambo la AJABU kwamba wale wanaoifanya Biblia kuwa MWALIMU WAO WA PEKEE, wangekuwa na kigeugeu hicho katika jambo hili kwa kufuata MAPOKEO ya Kanisa Katoliki?"
Mojawapo ya changamoto kuu kuliko zote ambayo imetupwa mbele ya Uprotestanti imo katika usemi wa Baba Enright, Rais wa Chuo cha Redemptor kule Marekani: "Lilikuwa ni Kanisa Takatifu la Katoliki lililobadili siku ya mapumziko toka Jumamosi kwenda Jumapili, siku ya kwanza ya juma. Nalo halikuwalazimisha tu wote kuishika Jumapili, bali liliwashurutisha watu wote kufanya kazi siku ya saba chini ya tamko la adhabu ya laana (anathema). Waprotestanti ... wanadai kuwa na heshima kuu kwa Biblia, lakini kwa tendo lao hili la ibada la kuiadhimisha Jumapili, wanakiri kwamba Kanisa Katoliki lina uwezo [wa kubadili siku]. Biblia inasema, 'Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.' Walakini Kanisa Katoliki linasema, HAPANA: Itakase siku ya kwanza ya juma, na tazama, ulimwengu wote uliostaarabika unasujudu kwa kicho na kuitii amri hii ya Kanisa Takatifu la Katoliki."
Yakupasa wewe kuijibu changamoto hiyo! Utamtii nani? Sikiliza maneno haya ya C.F. Thomas, Katibu Mkuu wa Kadinali Gibbons akijibu barua inayohusu badiliko la Sabato: "Ni kweli Kanisa Katoliki linadai kwamba badiliko hilo lilikuwa kitendo chake. Na kitendo hicho ni ALAMA [MARK] ya uwezo na mamlaka ya Uongozi wa Kanisa [Katoliki] katika masuala ya kidini." Kwa hiyo mambo yanakuwa wazi ----- Mungu anasema kwamba Yeye ni Mungu wa kweli; ametupa Sabato kama Muhuri wa Mamlaka Yake kama Muumbaji wa vyote. Kwa kuitunza Sabato tunaitambua mamlaka Yake kama Mungu wa kweli. Walakini, Kanisa Katoliki linajitokeza na kusema kweli maneno kama haya: "Hapana, usiitakase Sabato; itakase siku ya kwanza ya juma [Jumapili]. Ni sisi tulioibadili, na badiliko hilo ni ALAMA ya uwezo wetu wa kutangua sheria na mamlaka ya Mungu."
Kwa hiyo, ALAMA YA MNYAMA ni JUMAPILI ya bandia ambayo kwayo mamlaka hii ya Mnyama inajitahidi kutaka itambuliwe kuwa ndiyo mamlaka iliyo kuu kuliko Muumbaji Mwenyewe. Alama, au Muhuri, ya Mamlaka ya Mungu [Sabato] imeondolewa na mahali pake imewekwa Alama ile [Jumapili] ambayo Upapa unadai kuwa ni mamlaka yake. Laiti dunia yote ingaliweza kuliona kwa wazi jambo hili kuu sana lililo mbele yetu leo! Ni kwa nani sisi tutatoa UTII wetu ----- je! ni kwa Mungu au ni kwa Mnyama? Tunapoelewa mambo yalivyo hasa inatupasa kufanya UAMUZI mkubwa sana ama kuitunza Sabato ya kweli na kuitambua Mamlaka ya Mungu; ama kuipokea Sabato ya Uongo [Jumapili] na kuyatambua madai ya Kanisa Katoliki. Mwishowe inatupasa kupokea MUHURI WA MUNGU au ALAMA YA MNYAMA. Kuna pande mbili tu ----- MUNGU au JOKA, KWELI au UONGO, BIBLIA au MAPOKEO.
Kitabu kilichochapishwa mwaka 1956 chenye kichwa cha "THE FAITH OF MILLIONS" ambacho kinapatikana sasa katika Duka la Vitabu la Kikatoliki kama kitabu cha kiada (textbook) kuhusu dini hii ya Katoliki kina usemi huu wa kusisimua katika ukurasa wake wa 473: "Walakini, kwa vile Jumamosi, sio Jumapili, imetajwa kwa wazi katika Biblia, je! si ajabu kwamba wale wasio Wakatoliki wanaojidai kuichukua dini yao moja kwa moja kutoka katika Biblia na sio kutoka kwa Kanisa hili, wanaitunza Jumapili badala ya Jumamosi? Naam, kusema kweli, ni kukosa msimamo; walakini badiliko hilo lilifanyika karibu karne kumi na tano kabla ya kuzaliwa Uprotestanti, na kufikia wakati ule desturi hii [ya kuitunza Jumapili] ilikuwa inafuatwa ulimwenguni kote. [Waprotestanti] wameiendeleza desturi hii, japokuwa imejengwa juu ya mamlaka ya Kanisa Katoliki, wala sio juu ya fungu lo lote la Biblia linaloeleweka wazi. Uadhimishaji huo [wa Jumapili] unabaki kuwa kumbukumbu ya Kanisa Mama ambalo kutokana nalo madhehebu zisizokuwa za Kikatoliki zilijitenga mbali nalo ----- ni sawa na mvulana anayekimbia toka nyumbani kwao, lakini ambaye bado amechukua mfukoni mwake picha ya mama yake, ama msokoto wa nywele zake [mamake]."
Pamoja na [usemi] huo juu ongeza changamoto hii ya Kadinali Gibbons katika gazeti la CATHOLIC MIRROR la Desemba 23, 1893: "Haki na busara inataka tukubali moja au jingine kati ya mambo haya mawili ya kuchagua: aidha UPROTESTANTI NA KUITAKASA JUMAMOSI, au UKATOLIKI NA KUITAKASA JUMAPILI. Maafikiano kati ya mambo hayo mawili hayawezekani.
WAPROTESTANTI WANAAFIKI
Labda unashangaa kwamba Makanisa ya Kiprotestanti yanafikiri nini juu ya mambo haya ambayo tumekuwa tukiyatafakari. Watasema wao wenyewe. Hapa yapo MAUNGAMO ya kweli ya makanisa yale juu ya hoja hii ya Sabato. Semi zote zimedondolewa kutoka kwa wawakilishi wenye mamlaka kubwa sana [wa makanisa ya Kiprotestanti]. Hapa kuna dondoo kutoka kwa Dkt. Edward T. Hiscox, mwandishi wa Kanuni ya Kanisa la Kibaptisti, "Palikuwapo na bado ipo amri ya kuitakasa siku ya Sabato, lakini siku ile ya Sabato sio Jumapili. Walakini, itasemwa na kwa kuonyesha furaha kiasi fulani, ya kwamba Sabato ilihamishwa toka siku ya saba kwenda siku ya kwanza ya juma.... Ni wapi inapoweza kupatikana kumbukumbu ya kitendo kama hicho? Sio katika Agano Jipya ----- sio kabisa.... Ni kweli, mimi nami najua vema ya kwamba Jumapili ilianza kutumika mapema katika historia ya Kikristo kama siku ya dini, kama tunavyojifunza kwa Mababa Wakristo, na kutoka katika vianzo vinginevyo. Lakini NI JAMBO LA KUSIKITISHA JINSI GANI ya kwamba inakuja ikiwa imetiwa ALAMA YA UPAGANI, na kubatizwa kwa jina la Mungu-jua, wakati ilipochaguliwa na kutumiwa na UASI ule wa Kipapa, na kurithishwa kama urithi mtakatifu kwa Uprotestanti!' (Imedondolewa kutokana na Karatasi la Mada iliyosomwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Wachungaji mjini New York uliofanyika Novemba 13, 1893). Kiongozi huyu mkuu wa Kibaptisti anafanya muhtasari katika sentensi chache wa yale yote yaliyokwisha kusemwa katika kurasa za kijitabu hiki.
Gazeti la Kanisa la Presbyterian liitwalo "CHRISTIAN AT WORK" lilisema hivi: "Wengine wamejaribu kujenga hoja ya uadhimishaji wa Jumapili juu ya amri ya Mitume, wakati Mitume hao hawakutoa amri yo yote hata kidogo juu ya suala hilo.... Ukweli ni huu, mara tu tunapotumia Maandiko halisi ya Biblia, WASABATO wanayo hoja bora sana." Toleo la Aprili 19, 1883. Gazeti la METHODIST THEOLOGICAL COMPENDIUM linasema hivi: "Ni kweli kwamba hakuna amri yo yote ya hakika kwa ubatizo wa watoto wachanga.... Wala hakuna [amri yo yote] kwa kuitakasa siku ya kwanza ya juma."
Dkt. W.R. Dale (Kanisa la Congregational) katika kitabu chake cha "THE TEN COMMANDMENTS,' uk.106,107, asema, "Ni wazi ya kwamba haidhuru kwa ukali au kwa bidii jinsi gani tunaweza kuitunza Jumapili, HATUITAKASI SABATO. Sabato ilianzishwa kwa amri maalum ya Mungu. Hatuwezi kudai amri kama hiyo kwa utunzaji wa Jumapili.... Hakuna mstari hata mmoja katika Agano Jipya unaodokeza kwamba tunaweza kupata adhabu yo yote kwa kuvunja utakatifu unaodhaniwa tu wa Jumapili."
Msimamo wa KILUTHERI, kama ulivyofunuliwa katika kitabu chao cha Augsburg Confession of Faith, unasema, "Utunzaji wa Siku ya Bwana (Jumapili) haujajengwa juu ya amri yo yote ya Mungu, bali juu ya mamlaka ya Kanisa." Mwakilishi wa Kanisa la Episcopal aitwaye Neander anaandika hivi katika kitabu chake cha HISTORY OF THE CHRISTIAN RELIGION AND CHURCH, ukurasa 186: "Sikukuu ya Jumapili, kama sikukuu zingine, ilikuwa ni amri ya wanadamu, na ilikuwa mbali na makusudi ya Mitume wale kuweka amri ya Mungu kwa njia kama hii, ilikuwa mbali nao na mbali na Kanisa lile la mwanzo la Mitume kuhamisha kanuni za [utunzaji wa] Sabato kwenda Jumapili."
Katika kitabu kile cha TEN RULES FOR LIVING kilichoandikwa na Clovis G. Chappell, twasoma maneno haya: "Tungepaswa kukumbuka kwamba Sabato ni zawadi ya Mungu kwa mwanadamu. Ni kweli tunatambua kwamba Sabato yetu [Jumapili] sio ile inayotunzwa na Wayahudi. Yao ilikuwa ni siku ya saba ya juma, ambapo yetu ni siku ya kwanza. Sababu ya kuiadhimisha siku hii ya kwanza badala ya siku ile ya saba haina msingi wa amri yo yote [ya Mungu] iliyo dhahiri. Mmoja atayachunguza bure Maandiko ili kutafuta kibali cha kubadili [siku ya ibada] toka siku ya saba kwenda ile ya kwanza. Wakristo wale wa zamani walianza kuabudu katika siku ile ya kwanza ya juma kwa sababu Yesu alifufuka toka kwa wafu siku ile. Kadiri miaka ilivyopita, siku hii ya ibada ikafanywa kuwa siku ya mapumziko pia, sikukuu iliyoamriwa na Serikali. Jambo hilo lilitokea katika mwaka ule wa 321. Kwa hiyo, Sabato yetu ya Kikristo [Jumapili], haitokani na amri yo yote [ya Mungu] iliyo dhahiri." Ukurasa 61.
ALAMA HII ITALAZIMISHWA
Tungeweza kuendelea kutoa semi kutoka kwa dazeni ya vianzo vya madhehebu mengine, lakini nafasi hairuhusu. Jibu lako ni lipi kwa mambo haya? Kwa wazi tumeona kwamba Mungu alitabiri kutokea kwa mamlaka ambayo ingejaribu kuibadili Sabato; historia inaandika ya kwamba mamlaka hiyo ilifanya jaribio hilo; mamlaka yenyewe inaungama kwamba ilijaribu kuibadili [Sabato]; na Waprotestanti nao wanaungama ya kwamba badiliko hilo lilifanyika. Ni wangapi watakaochukua msimamo wao upande wa Biblia?
Kwa kasi sana ulimwengu unaukaribia wakati ule SABATO itakapokuwa ni JARIBIO KUU [KIPIMO KIKUU] LA UTII. Madai yake yatawekwa mbele ya wakazi wote wa ulimwengu huu. Wakati ule, mambo yatakapowekwa wazi, mtu mmoja mmoja ataupokea MUHURI WA MUNGU au ALAMA YA MNYAMA. Kitabu cha Ufunuo kinaeleza juu ya TANGAZO LA AMRI YA MWISHO kutoka kwa Serikali [zote] za ulimwengu huu ambalo litataka KULAZIMISHA ALAMA HII [YA MNYAMA ----- JUMAPILI] juu ya ulimwengu WOTE. "Naye awafanya WOTE, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, WATIWE CHAPA [ALAMA] katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze KUNUNUA wala KUUZA, isipokuwa ana chapa [alama] ile, yaani, jina la Mnyama yule, au hesabu ya jina lake." Ufunuo 13:16,17.
Ni dhahiri kwamba hakuna aliyepata ALAMA hiyo [sasa] mpaka hapo ITAKAPOLAZIMISHWA JUU YA WATU WOTE kwa njia ya kupitishwa Bungeni kama Sheria ya Serikali za wanadamu. Hapo ndipo SABATO YA KWELI na JUMAPILI YA UONGO zitakapofunuliwa kwa wazi kabisa hata hakuna atakayekwepa kufanya UAMUZI ----- uamuzi wa KUITUNZA SABATO YA KWELI kwa moyo na mkono wake, au KUITII SABATO YA UONGO [JUMAPILI] YA PAPA. Katika sura inayofuata utajifunza jinsi ya kulitambua taifa litakaloiongoza dunia [yote] kuipokea Jumapili ya Uongo, na litakalotafuta kuilazimisha alama ile ya utii kwa Papa [Jumapili] kwa kutumia NGUVU [za dola].